Habari
Ziara ya Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Chuo cha Diplomasia(CFR) kimeagizwa kufanya tafiti mahsusi za kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali kwenye jamii hususani za kistratejia na kiintelijensia na kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa chuo hicho.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) alipotembelea chuo hicho na kuzungumza na watumishi wake.