emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AZINDUA MAONYESHO YA 12 YA KIMATAIFA YA BIASHARA ZANZIBAR (ZANZIBAR INTERNATIONAL TRADE FAIR – ZITF)


Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla,amefungua rasmi Maonyesho ya Biashara  ya Kimataifa ya 62 ya Zanzibar yanayoendelea katika viunga vya maonyesho vya Nyamanzi, Fumba mjini Unguja.

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Makamu wa Pili wa Rais amesisitiza umuhimu wa maonyesho hayo kama chombo cha kukuza biashara, kuongeza fursa za uwekezaji na kuinua sekta ya uzalishaji hasa kwa wajasiriamali wa ndani. 

Alieleza kuwa serikali itaendelea kuwa miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa biashara ndogo, za kati na kubwa ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa uchumi wa visiwa vya Zanzibar na Pemba.

Mheshimiwa Abdullah ametembelea mabanda yaliyoshiriki maonyesho hayo ikiwa ni pamoja na  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Taasisi zake za AICC,APRM na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt .Salim Ahmed Salim.

Katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Abdullah Abdullah alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi  wa Afisi ya Mambo ya Nje Zanzibar Bw. Ally Ally na wafanyakazi wa Wizara walioko katika ofisi hiyo.

Mheshimiwa Abdullah amewapongeza watumishi wa Wizara na taasisi zake kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao.

Naye Mkurugenzi wa Maonyesho hayo amewataka wadau walioshiriki maonesho hayo kutumia fursa hiyo ya kipekee kuuza bidhaa, kutafuta washirika wa kibiashara na kupanua mitandao ya uwekezaji kwa kuwa maonyesho hayo ni jukwaa muhimu la kukuza soko la ndani na nje ya nchi.

Maonesho hayo yanashirikisha zaidi ya taasisi 316 kutoka serikalini, kampuni binafsi na washirika wa kimataifa yatamalizika Januari 16,2026.