Katika mazingira ya kimataifa yanayobadilika kwa kasi, Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim kinatumika kama kitovu cha mafunzo ya kitaaluma, tafiti zenye mwelekeo wa kisera na majadiliano yenye tija. Katika kujibu mahitaji ya diplomasia mpya yenye masuala mtambuka na yaliyochangamana, Programu zetu zimebuniwa kukuza umahiri wa uchambuzi, uongozi wenye maadili, na ujuzi wa vitendo unaohitajika kukabiliana na changamoto mpya za kidiplomasia na maendeleo.
Kwa kuzingatia dira ya Taifa ya Maendeleo, Kituo kinatoa mchango katika kuandaa Viongozi wenye weledi na uwezo wa kuendeleza diplomasia ya uchumi, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, na kulinda maslahi ya taifa katika jitihada za kufikia maendeleo endelevu.
Kupitia ushirikiano wa kimkakati na kubadilishana maarifa, Kituo kinaendelea kuunga mkono ushirikiano wa kikanda na ushiriki wenye tija katika jukwaa la kimataifa. Tunaendelea kujizatiti katika kujenga jamii ya wataalamu wenye uwezo wa kuchangia kikamilifu katika mwelekeo wa Tanzania kimataifa na hadhi yake duniani.
Tumejizatiti katika kuendeleza ubora wa hali ya juu katika nyanja za diplomasia, uhusiano wa kimataifa na uongozi wa kimkakati katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tukiongozwa na misingi ya Sera yetu ya Mambo ya Nje, tunaendelea kuimarisha uwezo wa taifa kushiriki kikamilifu na kwa ufanisi katika masuala ya kikanda na kimataifa.
Karibu uperuzi tovuti yetu, ambayo ninaimani itakuwa na manufaa kwako
Karibu!.
Higher Diploma Students
Programmes Offered
Employees
Wanafunzi wa Diploma