Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kituo cha Uhusiano wa kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim
Sera ya Faragha

Sera ya Faragha

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.Salim Ahmed Salim kinaichukulia faragha ya wateja na wanaotembelea tovuti yetu na watumiaji wa mifumo yetu kwa umuhimu mkubwa. Sera hii inaeleza hatua tunazochukua kuhifadhi na kulinda faragha yako unapotembelea au kuwasiliana na tovuti yetu au wafanyakazi. Tunakusanya na tunaweza kutumia baadhi ya taarifa kwa ajili ya kuboresha huduma zetu kwa wateja na wadau wetu mbalimbali.

Tunachukua hatua za maksudi za kiusalama kulinda taarifa zote dhidi ya watu wasiohusika nazo au uhariri, usambazaji au ufutaji wa taarifa bila idhini. Hatua hizi ni pamoja na mapitio ya mara kwa mara ya taarifa tunazoweka mtandaoni, uhifadhi na uchakataji wa taarifa hizo.