Majukumu Yetu Ya Msingi
Majukumu haya yanaongoza shughuli zetu za kila siku na yanafafanua namna tunavyowahudumia wanafunzi na wadau
Ukuzaji wa Diplomasia
Kukuza uelewa wa kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa kutoa fursa za kujifunza masuala ya kimataifa pamoja na mafunzo kuhusu misingi, taratibu na mbinu za diplomasia.
Mafunzo
Kuandaa na kutoa programu za mafunzo katika masuala yanayohusiana na mahusiano ya kimataifa na diplomasia kadri Baraza la Uongozi litakavyoelekeza.
Ushauri Elekezi
Kutoa huduma za ushauri elekezi na huduma nyingine za kitaalamu kwa Serikali pamoja na taasisi au mashirika mengine yatakayopata idhini ya Baraza la Uongozi.
Ushauri Mahsus
Kufanya tafiti kuhusu changamoto na mahitaji katika maeneo mbalimbali yaliyochaguliwa na kutathmini matokeo ya programu zake za mafunzo.
Kuandaa Makongamano ya Kidiplomasia
Kudhamini, kuandaa au kuwezesha mikutano, makongamano na semina kuhusu masuala yaliyo ndani ya wigo wa shughuli za Kituo.
Machapisho
Kuratibu uchapishaji na usambazaji wa machapisho na taarifa mbalimbali zinazotokana na kazi, tafiti na shughuli za Kituo