emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

CFR – Tanzania na CMI- Finland zimesaini Hati ya Makubaliano ya Mashirikiano (MoU)


Dkt. Felix Wandwe, ndc Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) na Balozi Jaane Taalas, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Amani ya Martti Ahtisaari (CMI) ya nchini Finland wamesaini Hati ya Makubaliano ya Mashirikiano (MoU) kuhusu kuwajengea uwezo watumishi wa CFR na Watanzania kwa ujumla katika masuala ya diplomasia, ulinzi wa amani, upatanishi na utatuzi wa migogoro.
Akizungumza baada ya kusainiwa kwa makubaliano haya Balozi Said Shaib Mussa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema ni muhimu kwa Taasisi hizi mbili kuharakisha kuanza kwa utekelezaji wa maeneo waliyokubaliana.
Kwa upande wake, Balozi Taalas ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuimarisha diplomasia na Finland, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) kwa kufanikisha kufanyika kwa semina ya Taasisi ya Amani ya Martti Ahtisaari (CMI), kusainiwa kwa hati ya makubaliano pamoja na mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Wizara, CFR, APRM na taasisi nyingine katika masuala ya ulinzi wa amani, upatanishi na utatuzi wa migogoro.
Hafla imefanyika katika ukumbi wa mikutano kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.