Hivi sasa tunaelekea kumaliza semester ya kwanza ya mwaka huu wa masomo, na wanafunzi wetu watatakiwa kufanya mafunzo kwa vitendo. Mafunzo kwa vitendo yamepangwa kuanza tarehe 9 Machi 2020 hadi tarehe 24 Aprili, 2020. Mafunzo kwa vitendo yanafanyika kwa kuzingatia taratibu na kanuni za NACTE. Ili kufanikisha takwa hilo, chuo kimejiwekea utaratibu wa kuwatafutia wanafunzi wetu nafasi kwenye Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali.