Habari
UJUMBE KUTOKA SEKRETARIETI YA APRM YA NAMIBIA UMETEMBELEA CFR

Mheshimiwa Balozi Lineekela J. Mboti, Mwakilishi Mkuu na Katibu Mtendaji wa APRM ya Namibia ameongoza Ujumbe kutoka Sekretarieti ya Mpango wa Hiari wa Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) ya Namibia. Akizungumza wakati wa kikao, Dkt. Jacob G. Nduye, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo amemshukuru Mheshimiwa Balozi Mboti na Ujumbe wake kwa Kukitembelea Kituo. Amesema Kituo kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kutoa mafunzo na ushauri, kufanya utafiri katika masuala ya Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa.
Kwa upande wake Mheshimiwa Mboti amesema lengo la ziara hii ya kukitembelea Kituo wanaamini kuna mengi ya kushirikiana baina ya nchi hizi mbili Namibia na Tanzania katika masuala ya kidiplomasia, kiutamaduni na kiuchumi kwa faida ya wananchi wa pande zote.