Habari
MAWAKILI WA SERIKALI WAPATA MAFUNZO YA ITIFAKI NA USTAARABU

Mafunzo ya Itifaki na ustaarabu kwa Mawakili wa Serikali (NPS) yaliyofanyika katika Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, jijini Dar es Salaam yamehitimishwa leo. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo katika masuala ya mawasiliano ya kitaaluma na mienendo ya kidiplomasia.
Akifunga mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Taaluma wa kituo hicho, Dkt. Anita Lugimbana, amewataka washiriki kutumia ujuzi walioupata kuboresha utendaji wao kazini, hasa katika kutekeleza majukumu yao ya kuiwakilisha serikali kwa weledi na heshima.
Dkt. Lugimbana pia amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu za kiitifaki katika shughuli rasmi za kiserikali, akibainisha kuwa ustaarabu na maadili ni nguzo muhimu katika kujenga taswira chanya ya utumishi wa umma.