Habari
RAIS SAMIA AMEMTEUA BALOZI RAMADHAN MUOMBWA MWINYI KUWA MWENYEKITI WA BARAZA LA UONGOZI LA KITUO CHA CFR KWA KIPINDI CHA PILI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 21 Februari, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, mheshimiwa Rais amemteua Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) kwa kipindi cha pili.