Habari
MAFUNZO YA ITIFAKI NA USTAARABU

TAFRIJA YA KUHITIMISHA MAFUNZO
Mafunzo ya Itifaki na Ustaarabu yaliyokuwa yakifanyika katika Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim yamehitimishwa leo . Mafunzo hayo yaliwaleta pamoja washiriki kutoka taasisi mbalimbali na wananchi kwa lengo la kuongeza uelewa na ujuzi juu ya mbinu bora za kiitifaki, mawasiliano yenye staha na ustaarabu katika mazingira ya kitaifa na kimataifa.
Wakufunzi walitoa msisitizo juu ya umuhimu wa weledi, heshima na uadilifu katika kuimarisha mahusiano ya kijamii, kitaaluma na kidiplomasia. Washiriki walipata nafasi ya kujifunza kwa vitendo namna ya kuendesha shughuli za kiserikali na kijamii kwa kuzingatia misingi ya itifaki na ustaarabu.
Akihitimisha mafunzo hayo,Kaimu Mkurugenzi Idara ya Taaluma,Utafiti, na Ushauri Dkt.Juma Kanua amewasihi wahitimu kuyatumia maarifa waliyopata katika utendaji wa kazi zao za kila siku na kuwa mabalozi wa maadili mema, mshikamano katika jamii,Kitaifa na Kimataifa.