Wigo
KUTOA MAFUNZO MBALIMBALI
Kituo kinaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kutoa mafunzo ya muda mrefu katika ngazi za Astashahada ya awali, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na Shahada za Uzamili.
Kwa upande wa kugha, Kituo kinatoa mafunzo ya lugha za kigeni zikiwemo Kireno, Kifaransa, Kichina, Kiarabu, Kihispaniola, Kikorea na lugha ya Kiswahili kwa Wageni. Aidha, mafunzo maalumu na kozi za muda mfupi katika masuala ya Uongozi wa kimkakati; Diplomasia; Uhusiano wa kimataifa; Stratejia; Usuluhishi wa migogoro na Ujenzi wa amani, yameendelea kutolewa kwa wadau mbalimbali wakiwemo watumishi kutoka Taasisi za umma na Sekta binafsi.
