emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

WATUMISHI WAMEASWA KUJENGA TABIA YA KUJITAFUTIA MAARIFA.


WATUMISHI WAMEASWA KUJENGA TABIA YA KUJITAFUTIA MAARIFA.

Watumishi mbalimbali kutoka Taasisi za Serikali wamehudhuria mafunzo ya migogoro na usuluhishi wa migogoro kwa muda wa siku tano (5) yaliyotolewa na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim.

Alipokuwa akifunga mafunzo hayo Dkt. Jacob Nduye Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha katika Kituo Cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim amesema "Ninawapongeza sana kwa kujitoa na kufanya maamuzi sahihi ya kuja kuhudhuria mafunzo haya,nafahamu mmeacha majukumu yenu na kuja katika mafunzo haya.Mimi naamini katika kujitafutia maarifa ,hivyo nawasihi watumishi wenzangu tuendelee kujijengea utaratibu wa kutafuta maarifa zaidi ili kuwa na ufanisi katika kazi zetu kwa maslahi  binafsi na Taifa kwa  ujumla. "

Watumishi hao wamesema mafunzo haya yamewafanya kuwa tofauti na walivyokuwa mwanzo,baada ya kupata mafunzo haya wamegundua mambo mbalimbali ambayo yatakuwa msaada mkubwa katika maisha yao na  utendaji wao wa majukumu ya kila siku.

Mafunzo haya yamelenga kuwapa maarifa watumishi hao katika kufahamu aina ya migogoro na namna ya usuluhishi wa migogoro katika ngazi ya familia,jamii ,kazi na Taifa kiujumla.