emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

Mitihani ya Muhula wa kwanza 2023/2024


Mitihani ya Muhula wa kwanza kufanyika 5 Februari 2024 hadi 16 2024

Wanafunzi wa Kituo cha Dkt.Salimu Ahmed Salimu wameanza kufanza mitihani ,ikiwa ni mitihani ya muhula wa kwanza katika mwaka wa masomo 2023/2024.

Mitihani hiyo imehusisha wanafunzi  katika level  mbalimbali ikiwa ni NTA Leve 4 ,NTA level 6,level 7,Level 8, na level 9 katika masomo mbalimbali, ikiwemo Lugha ya kifarasa, kihispaniola,kiarabu,kichina kikorea,kireno na ubobezi katika eneo la Uhusiano wa kimataifa na Diplomasia
Hayo ameyasema Mkuu wa sehemu ya Mitihani ndugu Frank Mbele kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mafunzo Dkt.Annita Lugimbana.
 
Ameongeza kwamba kazi ya mitihani na usimamizi wake inahitaji ushirikiano wa Kutosha kutoka kwa sehemu nyingine kwa umuhimu ili ifanyike kwa uweledi, hivyo  Ofisi ya Mkurugenzi wa Mafunzo na sehemu ya mitihani ,sehemu ya   Taaluma,sehemu ya udhibiti Ubora, sehemu ya uhasibu na waadhili wanashirikiana vizuri katika kufanikisha dhumuni hilo.

Akiongea kuhususiana na Wanafunzi wa Shahada ya kwanza  ambao wamebaki na muhula mmoja ili wamalize  amesema," hawa ni vijana wamejifunza Mambo mengi katika eneo la uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia tunatarajia mafunzo waliyo yapata yatawawezesha kwenda kuhudumia Umma, katika taasisi za serikali ,katika sekta binafsi, lakini pia katika kujiajiri.

Ndugu Frank Mbele alimaliza kwa ushauri kwa Wanafunzi kuongeza Umakini  katika mitihani yao ili wafanye vizuri na mwisho  wafanikiwe katika Ndoto zao.