Habari
MAHAFALI YA 26 YA KITUO CHA UHUSIANO WA KIMATAIFA CHA DKT. SALIM AHMED SALIM.

SERIKALI YAKITAKA KITUO
CHA UHUSIANO WA KIMATAIFA CHA DKT. SALIM
KUTOA ELIMU BORA YA DIPLOMASIA, STRATEJIA
Serikali imekitaka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha
Dkt. Salim Ahmed Salim kuhahikisha kinaendelea kutoa
elimu bora ya Uhusiano wa Kimataifa, Diplomasia na
Stadi za Stratejia.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.)
ambaye alimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January
Makamba (Mb.) ametoa agizo hilo katika mahafali ya 26
ya Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim
Ahmed Salim na kuwatunuku vyeti wahitimu 1,008.
Wahitimu hao wametunukiwa vyeti katika maeneo ya
Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia, Diplomasia ya
Uchumi, Usimamizi wa Amani na Migogoro na Utawala wa kimkakati
"Wizara inapenda kusisitiza umuhimu wa Kituo
kuendelea kuelimisha Taifa kupitia mijadala na
makongamano kwa lengo la kupanua uelewa wa
masuala mbalimbali. Kituo kinapaswa pia kuendelea
kusimamia na kutekeleza Majukumu ya Msingi ya
kuanzishwa kwake ambayo yanajumuisha Taaluma,
Utafiti na Ushauri Elekezi," alisema Balozi Mbarouk.
Balozi Mbarouk aliongeza kuwa ni vyema Kituo
kikaboresha progamu zake ili kukidhi mahitaji ya Wizara,
Nchi na watanzania kwa ujumlawake,ambapo alishauri
kuwa Kituo kiendelee kutoa elimu ya masuala
mbalimbali yanayohusiana na Uhusiano wa Kimataifa,
Diplomasia ya Uchumi na Stratejia kwa taasisi za
Serikali na sekta binafsi ili kusaidia kukuza ujuzi wa
wananchi wetu.
"Naelekeza usimamie utekelezaji wa mabadiliko
yanayoendelea kama ilivyopendekezwa na Kamati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki na taasisi zilizo chilli yake," Aliongeza Balozi
Mbarouk.
Aidha ,Dkt,Jacobu nduye Kaimu mkurugenzi wa utawala na fedha katika kituo cha Dkt Salim Ahmed Salimu akimshukuru Mungu kwa kufanikisha tukio hilo la maafali, ameeleza kuhusu kituo hicho kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji katika Diplomasia ya uchumi. Ameeleza pia kuhusu mafunzo mbalimbali yanayotolewa katika Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.Salimu Ahmed Salimu ,ikiwa ni ya muda mrefu na ya muda mfupi katika ngazi ya Astashahada ya awali ya Uhusiano wa kimataifa na Diplomasia,Astashahada ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia,Stashahada ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia,Stashahada ya juu ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia,Shahada ya Uhusiano wa Kimataifa,Stashahada ya Uzamili ya mahusiano ya Kimataifa,Stashahada ya Uzamili katika Amani na Menejiment ya migogoro na Shahada ya Uzamili ya utawala wa kimkakati.
‟Kituo kinatoa mafunzo ya lugha mbali mbali za kigeni ,ikiwemo kireno ,kichina ,kiarabu,kihispania,kifaransa na kikorea .Pia chuo hicho kinatoa mafunzo maalumu ya muda mfupi kwa wadau mbalimbali wakiwemo watumishi wa Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki”.alieleza Dkt. Jacob Nduye.