emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

CHUO CHA ULINZI WA TAIFA CHA JAMUHURI YA KIARABU CHA MISRI KUPATA MAFUNZO KATIKA KITUO CHA UHUSIANO WA KIMATAIFA CHA DKT.SALIMU AHMED SALIMU.


CHUO CHA ULINZI WA TAIFA CHA JAMUHURI YA KIARABU CHA MISRI KIMEPATA MAFUNZO KATIKA KITUO CHA UHUSIANO WA KIMATAIFA CHA DKT.SALIMU AHMED SALIMU.

Maafisa kutoka Chuo cha Taifa cha Jamhuri ya Kiarabu cha Misri wamepatiwa  mafunzo ya siku moja kutoka Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salimu yaliyolenga  kuwapatia maafisa hao uelewa katika masuala yanayohusu ulinzi, usalama na dipolomasia.

Akizungumza katika mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Kituo cha Uhusiano wa Kitaifa cha Dkt Salim Ahmed Salim, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha , Dkt. Jacob Nduye amewahakikishia maafisa hao kuwa watapata wasaa wa kujifunza mambo mengi ambayo ni muhimu katika kukuza diplomasia hususani katika masuala ya ulinzi na usalama ambayo ni muhimu kulingana na mabadiliko ya kiuchumi duniani.

“Natumia fursa hii kuwakaribisha katika kituo hiki ambacho kina historia ya muda mrefu Afrika katika masuala ya diplomasia, uwepo wenu hapa kutawawezesha kujua mambo mbalimbali ambayo nina hakika yatawasaidia kuendelea kuboresha utendaji kazi wenu” ameongeza Dkt. Nduye.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo katika chuo hiicho Bw. Godwin Gonde amesema Tanzania na Misri zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu hivyo Ujio wa ugeni huu utajifunza  mambo mengi pamoja na sera ya mambo ya nje ya Tanzania na  uhusiano uliopo kati ya Sera ya mambo ya nje na  maswala ya ulinzi na usalama  ambayo jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayafanya.

Naye, Mkuu wa Msafara kutoka Chuo cha Taifa cha Jamhuri ya Kiarabu cha Misri Brigedia Jenerali Hossam El-Din Mohamed Mustafa El-Sherbiny ameushukuru uongozi wa chuo hicho kwa mapokezi waliyopata na kuahidi kuwa watayatumia mafunzo hayo kuboresha utendaji kazi ili kuendelea kulinda amani ya nchi yao na dunia kwa ujumla.