emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

WANAFUNZI NA WAKUFUNZI  KUTOKA CHUO CHA KIJESHI CHA UKAMANDA NA UNADHIMU CHA ZIMBABWE WAMETEMBELEA KITUO CHA UHUSIANO WA KIMATAIFA CHA DKT. SALIM AHMED SALIM


Ujumbe wa Wanafunzi na Wakufunzi 31 kutoka Chuo cha Kijeshi cha Ukamanda na Unadhimu cha Zimbabwe wakiongozwa na Naibu Kamanda, GC  Joyce Maeresera, leo Jumatatu tarehe 29 Julai 2024  wametembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim(CFR).
Akizungumza wakati wa ziara hii Naibu Kamanda GC Joyce Maeresera amesema lengo la ziara hii ni kujifunza masuala ya kiulinzi, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Dkt. Felix Wandwe, ndc pamoja na mambo mengine yaliyofanyika wakati wa ziara hii,  ameushukuru Uongozi wa Ujumbe huu kutoka Zimbabwe kwa ziara yao ya  kukitembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR).
 Dkt. Felix Wandwe, ndc  amesema Kituo kinatoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu katika masuala ya Diplomasia, Uhusiano wa Kimataifa, Stadi za Stratejia, Usuluhishi wa migogoro na Ujenzi wa Amani.