emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

BALOZI WA MAREKANI NCHINI TANZANIA AMETEMBELEA KITUO CHA UHUSIANO WA KIMATAIFA CHA DKT.SALIM AHMED SALIM.


Balozi wa Marekani nchini Tanzania, mheshimiwa Michael Battle, leo Alhamis tarehe 23 Mei 2024 ametembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR).
Akiwa katika Kituo hicho, Mheshimiwa Balozi Battle amekutana na kuzungumza na Dkt. Felix Wandwe, ndc Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Dkt. Salim Ahmed Salim, kutoa muhadhara wa kidiplomasia kwa baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa Kituo pamoja na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali aliyoulizwa na wanafunzi.