emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

WAFANYAKAZI WA KITUO CHA DKT.SALIM AHMED SALIM WAMEPATA MAFUNZO YA HUDUMA ZA PSSSF KWA NJIA YA MTANDAO


WAFANYAKAZI WA KITUO CHA DKT.SALIM AHMED SALIM  WAMEPATA MAFUNZO YA  HUDUMA ZA PSSSF KWA NJIA YA MTANDAO.

Watumishi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa  cha Dkt.Salim Ahmed Salimu  leo wamepata mafunzo ya namna ya kupata huduma zinazotolewazo na mfuko wa hifadhi ya jamii wa utumishi wa umma (PSSSF) kwa njia ya mtandao.

Alipofungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa kituo Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt Salim Ahmed Salim, Dkt.Jacob Nduye amesema "kutokana na changamoto mbalimbali walizokuwa wanazipitia  watumishi wanapohitaji huduma zitolewazo na mfuko huo,hivyo mafunzo hayo yataleta tija kwa watumishi na kuondoa usumbufu walikuwa wakiupata kipindi  walipokuwa wakihitaji  huduma katika mfuko huo .

 

Kwa upande wa mtekelezaji wa Mafunzo hayo ndugu Thadeus Rweyamba  amesema"mafunzo hayo yamekusudia kuondoa urasimu kwa kuboresha huduma  zake katika kutoa huduma bora kwa njia ya mtandao badala ya mfumo uliokuwa unatumika kwa njia ya karatasi .

Ameongeza kwa kusema mfumo huo utawasaidia wanachama  kupata huduma mbalimbali ikiwemo  ufuatiriaji wa mafao na huduma nyingine zinazotokana na mfuko huo.