emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

ZIARA YA MHESHIMIWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI MHESHIMIWA BALOZI MAHMOUD THABITI KOMBO (Mb) CFR.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb) leo ametembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimaifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) na kuzungumza  na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Kituo Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo, Dkt. Felix Wandwe, ndc, baadhi ya Wakuu wa Idara na Maafisa Waandamizi wa Wizara na Kituo cha CFR.
Mheshimiwa Balozi Kombo alipata fursa ya kutembelea  mradi wa ujenzi wa vyumba vya mihadhara pamoja na kuzungumza na washiriki   wa mafunzo ya muda mfupi kutoka Taasisi za Umma na Sekta binafsi kuhusu Stadi za Uongozi na Majadiliano.