Habari
MAFUNZO KUHUSU ELIMU YA RUSHWA NA UKIMWI YAMETOLEWA LEO KWA WAFANYAKAZI WA CFR

leo wafanyakazi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.Salim Ahmed Salim wamepata mafunzo kuhusiana na Elimu juu ya Rushwa na Ukimwi.
Katika mafunzo yaliyohusiana na Rushwa ambayo yametolewa na maafisa kutoka Takukuru ambao ni Bi.Neema Kilongo na Bi.Sabina Isuja yamelenga kumuelimisha mfanyakazi namna ya kuepuka rushwa na kuzuia rushwa katika eneo la kazi na kijamii wakisisitizwa kuishi kwa Imani ikihusishwa na hofu kwa Mwenyezi Mungu.
Aidha Katika mafunzo yaliyotolewa na Dkt.Lilian Mnzava kutoka TACAIDS yamelenga kumuelimisha mfanyakazi namna ya kuepuka mazingira hatarishi yanayoweza kupelekea ongezeko la maambukizi ya Ukumwi katika eneo la Kazi na kijamii,pia kuangalia namna sahihi ya matumizi ya chakula kwa kula chakula bora na kuepuka ulaji wa vyakula hatarishi kiafya.