emblem

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim

Habari

Mafunzo ya Muda Mfupi ya Itifaki na Ustaarabu Yaanza leo katika Kituo cha Dkt. Salim Ahmed Salim


Mafunzo ya muda mfupi kuhusu itifaki na ustaarabu yameanza leo katika Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim. Mafunzo haya yanawalenga watumishi wa umma na wadau wa mahusiano ya kimataifa kwa lengo la kuwaongezea maarifa na stadi kuhusu misingi ya itifaki, ustaarabu na mawasiliano yenye weledi katika mazingira ya kikazi na kidiplomasia.