Katika jitihada za kuimarisha uwezo wa utafiti na machapisho ya kitaaluma, Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dr. Salim Ahmed Salim (CFR) kimeanza rasmi mafunzo ya Uandishi wa Kitaaluma (Academic Writing Training Workshop)kwa watumishi wake leo yanayofanyika, katika Ukumbi Mdogo wa Bunge, jijini Dar es Salaam.
Warsha hiyo imefunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Taaluma, Utafiti na Ushauri elekezi wa Kituo Cha Uhusiano wa Kimataifa Dkt. Anita Lugimbana. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Dkt. Lugimbana amesisitiza kuwa uandishi bora wa kitaaluma ni nyenzo muhimu katika kukuza hadhi ya kituo hicho kama kitovu cha diplomasia na masuala ya kimataifa. Amebainisha kuwa kuwajengea uwezo watumishi kutasaidia kuongeza idadi na ubora wa machapisho yanayotolewa na kituo hicho.
Mafunzo haya yanatolewa na Mkurugeni wa huduma za maktaba katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam,Prof.Kelefa Tende Mwantimwa ambaye katika mafunzo haya anafundisha maswala mbalimbali katika utaalamu wa uandishi wa tafiti pamoja na mbinu za kuandaa maandiko yenye viwango vya kimataifa na kuzingatia maadili ya kitaaluma.
Kama taasisi inayoshika usukani katika masuala ya diplomasia na sera za kimataifa, uwezo wa watumishi wake kutoa tafiti zenye mashiko ni kipaumbele cha kwanza. Mafunzo haya ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa CFR kuhakikisha kuwa watumishi wake wanakuwa na sifa stahiki za kushindana na kutoa mchango wa kitaluma duniani kote.
Mafunzo haya yatawawezesha watumishi kupata uelewa zaidi kupitia mijadala ya kina kuhusu changamoto na fursa zilizopo katika uandishi. Mafunzo haya yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 9 Aprili, 2026 huku yakiacha alama ya kimkakati katika kukuza taaluma ndani ya Kituo cha Dkt. Salim Ahmed Salim.
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim ( CFR), kimetoa wito...
Mafunzo ya muda mfupi kuhusu Itifaki za Mashirika na Uhusiano wa Serikali (Corpo...
Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania, Mheshimiwa Yordenis Despaigne Vera, l...
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, kimepokea ujumbe kut...
Mapema Novemba 17, 2025 Wazazi na watoto wao wakiwa na nyuso zenye matumaini ya...