Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kituo cha Uhusiano wa kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim
BALOZI WA CUBA NCHINI TANZANIA ATOA MHADHARA KATIK...

BALOZI WA CUBA NCHINI TANZANIA ATOA MHADHARA KATIKA KITUO CHA DKT. SALIM AHMED SALIM

19 Jun, 2026
BALOZI WA CUBA NCHINI TANZANIA ATOA MHADHARA KATIKA KITUO CHA DKT. SALIM AHMED SALIM

Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania, Mheshimiwa Yordenis Despaigne Vera, leo ametembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim na kutoa Mhadhara kwa jumuiya ya Kituo ikijumuisha wafanyakazi, wahadhiri, na wanafunzi.


Mhadhara huo ulikuwa na  mada isemayo: "Uhusiano wa Kihistoria Kati ya Tanzania na Cuba: Mtazamo wa Kisiasa, Kiuchumi na Kijamii nchini Cuba." Kupitia mada hiyo, Balozi Vera alieleza chimbuko la uhusiano imara wa kidiplomasia baina ya nchi hizo ulioasisiwa na viongozi wakuu wa mataifa haya, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Fidel Castro. 


Aidha, ametoa taswira ya sasa ya hali ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii nchini Cuba, pamoja na fursa mpya za ushirikiano katika sekta za afya, elimu, na maendeleo ya kijamii.Ujio wa Balozi wa Cuba katika Kituo unatajwa na uongozi wa Kituo kuwa ni fursa adhimu kwa wanafunzi, wahadhiri na jumuiya ya Kituo kujifunza kuhusu hali ilivyo nchini Cuba kutoka kwa mwakilishi  wake.


Balozi Vera alitumia muhadhara huo kushukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea na mshikamano na Cuba katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa kupinga vikwazo dhidi yake, akisema hatua hiyo inaonesha undugu na mshikamano wa kihistoria uliopo kati ya mataifa hayo mawili.
Akifunga mhadhara huo, Kaimu Mkurugenzi wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa kituo hicho, Bw. Avit Chami, alimshukuru Balozi Vera kwa kuwasilisha mada hiyo na kuwapatia wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa kituo taarifa na ufahamu mpana kuhusu hali halisi ya Cuba na mwelekeo wa mahusiano yake na Tanzania.Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania,