Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kituo cha Uhusiano wa kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim
KITUO CHA UHUSIANO WA KIMATAIFA CHA DKT. SALIM AHM...

KITUO CHA UHUSIANO WA KIMATAIFA CHA DKT. SALIM AHMED SALIM-CFR, CHAPOKEA UJUMBE KUTOKA CHUO CHA JESHI LA ANGA CHA NIGERIA

12 Jun, 2026
KITUO CHA UHUSIANO WA KIMATAIFA CHA DKT. SALIM AHMED SALIM-CFR,  CHAPOKEA UJUMBE KUTOKA CHUO CHA JESHI LA ANGA CHA NIGERIA

Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, kimepokea ujumbe kutoka Chuo cha Jeshi la Anga cha Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria kama sehemu ya ziara yao ya mafunzo nchini Tanzania. 

Ujumbe huo ulipokelewa na kukaribishwa na Dkt. Anita Lugimbana, Kaimu Mkurugenzi wa Kituo akiambatana na viongozi wengine waandamizi wa Kituo hicho. Katika salam zake za ukaribisho, Dkt. Lugimbana alieleza kuwa ziara hiyo ni ya kihistoria na inadhihirisha urafiki na ushirika wa kimkakati baina ya Tanzania na Nigeria. 

"Uhusiano wa uwili baina ya nchi hizi mbili umekuwepo tangu wakati wa ukombozi wa bara la Afrika na umeendelea kuimarika hata baada ya ukoloni na sera za ubaguzi wa rangi (zilizokuwepo nchini Afrika Kusini), kutokana na alama zilizoachwa na waasisi wa mataifa yetu. Kwa kuwa Nigeria ina historia ya muda mrefu na Tanzania, hususan wakati wa Nchi za Mstari wa Mbele, tunaheshimu na kuenzi ushirikiano na urafiki huo na tuko tayari kuuendeleza zaidi" aliongeza Dkt. Lugimbana. 

Kwa upande wa Mkuu wa Msafara wa Chuo cha Jeshi la Anga cha Nigeria, Commodore Sheshu Mohamed Chindo, alieleza lengo la ziara yao nchini Tanzania na katika Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Salim Ahmed Salim; aliushukuru uongozi wa Kituo kwa mapokezi mazuri na kwa mawasilisho mazuri yaliyofanywa kwa ujumbe wake. Alisema " Kilikuwa ni kipindi kizuri chenye mjadala unaojenga uliojielekeza kwenye mada isemayo ""The Intergrating Emerging Technolgies for National Security".