Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kituo cha Uhusiano wa kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim
MAFUNZO YA ITIFAKI NA UHUSIANO WA KIMKAKATI NA SER...

MAFUNZO YA ITIFAKI NA UHUSIANO WA KIMKAKATI NA SERIKALI KATIKA KITUO CHA DKT. SALIM AHMED SALIM (CFR)

19 Jun, 2026
MAFUNZO YA ITIFAKI NA UHUSIANO WA KIMKAKATI NA SERIKALI KATIKA KITUO CHA DKT. SALIM AHMED SALIM (CFR)

Mafunzo ya muda mfupi kuhusu Itifaki za Mashirika na Uhusiano wa Serikali (Corporate Protocol and Government Relations) yaliyokuwa yakifanyika katika Kituo cha Uhusiano wa Kigeni cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) yamehitimishwa rasmi leo kwa mafanikio makubwa.

Mafunzo hayo yamefungwa na Dkt. Jacob Nduye, ambaye aliwashukuru washiriki kwa kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika kujifunza mbinu mbalimbali za kiitifaki na usimamizi wa mahusiano ya kimkakati na Serikali.

Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo, Dkt. Nduye alisema kuwa uelewa wa itifaki za mashirika na mahusiano mazuri na Serikali ni nyenzo muhimu kwa taasisi za umma na binafsi katika kufanikisha majukumu yao na kujenga ushirikiano wenye tija.

Mafunzo hayo yaliwashirikisha washiriki kutoka mashirika binafsi na taasisi za umma, yakilenga kuwajengea uwezo wa kuimarisha mahusiano ya kimkakati, kuelewa misingi ya kiitifaki, na kuboresha mawasiliano pamoja na utendaji kazi wa kila siku na Serikali.

Mafunzo haya ni sehemu ya mkakati endelevu wa Kituo cha Dkt. Salim Ahmed Salim wa kutoa mafunzo ya muda mfupi yenye tija kwa wadau mbalimbali, kwa lengo la kueneza stadi za kidiplomasia, mbinu za majadiliano na mifumo ya kisasa ya kiitifaki kwa sekta zote za maendeleo nchini.