Mheshimiwa Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed, Balozi wa Comoro nchini Tanzania, leo 2Julai 2026 ametoa Mhadhara kuhusu " Mchango wa Tanzania uliosaidia kupatikana kwa Uhuru wa Comoro" tarehe 06/7/1975.
Akifungua Mhadhara huu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, mheshimiwa Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb) amesema mashirikiano yaliyopo kati ya Tanzania na Comoro ni ya muda mrefu na yameendelea kuimarika katika nyanja za Kidiplomasia; Elimu; Uchumi; Biashara na Sekta ya Afya.
Kwa upande wake, mheshimiwa Balozi Dkt. Ahamada amesema Comoro inatambua mchango mkubwa uliotolewa na Tanzania wakati wa kutafuta uhuru uliopatikana mwaka 1975. "Tumefanya Mhadhara huu kwa lengo la kuwakumbusha vijana wetu wanaosoma hapa historia na mchango mkubwa uliotolewa na nchi hii-Tanzania katika kusaidia kupatikana kwa Uhuru wa Comoro na mashirikiano yaliyopo kwa faida ya wananchi wa pande zote mbili". amesema Balozi Ahamada.
Mhadhara huu ni sehemu ya shughuli za Maadhimisho ya Miaka 51 ya Uhuru wa Comoro, umefanyika Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) na kuhudhuriwa na baadhi ya waheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania: wawakilishi wa Jumuiya na Taasisi za Kimataifa, Viongozi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wanataaluma, Wafanyakazi, Wanafunzi na Jumuiya ya Kituo (CFR).
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim ( CFR), kimetoa wito...
Mafunzo ya muda mfupi kuhusu Itifaki za Mashirika na Uhusiano wa Serikali (Corpo...
Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania, Mheshimiwa Yordenis Despaigne Vera, l...
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, kimepokea ujumbe kut...
Mapema Novemba 17, 2025 Wazazi na watoto wao wakiwa na nyuso zenye matumaini ya...