Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim ( CFR), kimetoa wito kwa vijana wenye sifa, watumishi kutoka Taasisi za Umma na Sekta Binafsi kuchangamkia fursa zilizopo za masomo ya muda mrefu na kozi za muda mfupi katika nyanja za Diplomasia, Uhusiano wa Kimataifa, Usuluhishi na Utatuzi wa Migogoro, ujenzi wa Amani, Stratejia, lugha za Kigeni na lugha ya Kiswahili kwa Wageni Ili wawe mahili na wenye weledi kitaaluma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko (CFR), Bw. Richard Cheyo amesema haya akiwa katika Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Taasisi zilizo chini yake, wakati wa Maonesho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2026 yanayofanyika katika viwanja vya Chinangali Park, Dodoma.
"CFR tupo katika viwanja vya Chinangali katika Maonesho yanayoendelea kwa lengo la kutoa elimu kwa wadau na wananchi kuhusu majukumu ya msingi yanayotekelezwa na Kituo ambayo ni taaluma, Utafiti, ushauri elekezi na programu maalum. Nachukua fursa hii kuwaomba vijana wenye sifa kuchangamkia fursa za kujiunga na masomo yanayotolewa na Kituo. Kituo kimeendelea kutoa mafunzo na kozi mbalimbali katika masuala ya Uhusiano wa Kimataifa, Diplomasia, Menejimenti ya Uhusiano wa Kimataifa, Amani na Menejimenti ya Migogoro, Diplomasia ya Uchumi na Utawala wa Kimkakati" amesema Bw. Cheyo.
Akizungumzia kuhusu Udahili- unaoendelea, amesema Dirisha la Udahili- ngazi ya Stashahada ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia lilifunguliwa mwishoni mwa mwezi Mei na litafungwa tarehe 10 Julai 2026, maombi yanafanyika kupitia mfumo wa Udahili- wa Kituo wa (https://oas.cfr.ac.tz). Waombaji wanakumbushwa kuijaza taarifa zao Kwa usahihi na kutunza kumbukumbu zao.
Dhamiri ya Kituo ni kutoa huduma Bora za kitaaluma kupitia Mafunzo, Utafiti na Ushauri Elekezi katika nyanja za Diplomasia na stadi za Stratejia katika ngazi za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa.
Mafunzo ya muda mfupi kuhusu Itifaki za Mashirika na Uhusiano wa Serikali (Corpo...
Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania, Mheshimiwa Yordenis Despaigne Vera, l...
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, kimepokea ujumbe kut...
Mapema Novemba 17, 2025 Wazazi na watoto wao wakiwa na nyuso zenye matumaini ya...
Balozi wa India nchini, Mheshimiwa Bishwadip Dey, amefanya ziara rasmi katika Ki...