Kituo cha Dkt. Salim Ahmed Salim cha Mahusiano ya Kimataifa (CFR) leo kimepokea ujumbe kutoka CMI – Martti Ahtisaari Peace Foundation ya Finland, ukiongozwa na Bi. Tiina Kukkamaa-Bah, Mkuu wa Kitengo cha Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Ziara hiyo imelenga kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo katika masuala ya diplomasia, usimamizi wa migogoro, upatanishi na ujenzi wa amani, pamoja na nafasi ya Tanzania katika kukuza amani na usalama wa kikanda na kimataifa.
Ziara hiyo ni mwendelezo wa ushirikiano ulioimarishwa kufuatia Semina ya Urithi wa Martti Ahtisaari iliyofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2025 na kutiwa saini kwa Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya CMI na CFR.
Ushirikiano huo unalenga kuendeleza maarifa, uzoefu na uwezo wa kitaasisi katika kukuza diplomasia ya amani na kutafuta suluhu za migogoro kupitia njia za mazungumzo na upatanishi.
Ujumbe kutoka Chuo cha Diplomasia cha Anwar Gargash (Anwar Gargash Diplomatic Ac...
Mafunzo maalum ya Diplomasia na Maadili ya Kazi (Diplomacy and Professional Etiq...
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) kimeandaa Konga...
DAR ES SALAAM: Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Sa...
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim ( CFR), kimetoa wito...