Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kituo cha Uhusiano wa kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim
UJUMBE KUTOKA CHUO CHA DIPLOMASIA CHA ANWAR GARGAS...

UJUMBE KUTOKA CHUO CHA DIPLOMASIA CHA ANWAR GARGASH (AGDA) WATEMBELEA CFR KWA AJILI YA KUBADILISHANA UZOEFU NA WANAFUNZI

18 Nov, 2026
UJUMBE KUTOKA CHUO CHA DIPLOMASIA CHA ANWAR GARGASH (AGDA) WATEMBELEA CFR KWA AJILI YA KUBADILISHANA UZOEFU NA WANAFUNZI

Ujumbe kutoka Chuo cha Diplomasia cha Anwar Gargash (Anwar Gargash Diplomatic Academy – AGDA) umetembelea Kituo cha Dkt. Salim Ahmed Salim cha Mahusiano ya Kimataifa (CFR) kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kushirikiana na wanafunzi wa CFR.

Ziara hiyo imetoa fursa kwa wanafunzi kutoka taasisi zote mbili kubadilishana maarifa, mitazamo na uzoefu wa kitaaluma katika masuala ya diplomasia na mahusiano ya kimataifa.

Aidha, ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kitaasisi na kukuza ushirikiano wa kitaaluma kati ya taasisi hizo mbili zinazojihusisha na mafunzo ya diplomasia.