Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kituo cha Uhusiano wa kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim
Mafunzo Ya Itifaki Na Ustaarabu Yaanza Katika Kitu...

Mafunzo Ya Itifaki Na Ustaarabu Yaanza Katika Kituo Cha Dkt. Salim Ahmed Salim.

29 Jun, 2026
Mafunzo Ya Itifaki Na Ustaarabu Yaanza Katika Kituo Cha Dkt. Salim Ahmed Salim.

 

DAR ES SALAAM: Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) Kama ilivyo katika jitihada zake za kuongeza  wigo  mpana wa  uelewa  wa maswala ya Kidiplomasia na Uhusiano wa Kimataifa,kimekuwa kikiendelea kutoa kozi za muda mfupi ambazo hufanyika kwa siku tano(5)na kozi za muda mrefu kuanzia mwaka mmoja(1)na zaidi kituoni hapo.

Katika jitihada  hizo endelevu kwa wadau mbalimbali nchini, Leo Kituo kinatoa mafunzo ya muda mfupi kuhusiana na  masuala ya Itifaki na Ustaarabu (Protocol and Etiquette). Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo watumishi katika sekta mbalimbali ili kuongeza ufanisi na weledi mahali pa kazi na katika jamii.

Mafunzo haya yamewakutanisha washiriki kutoka maeneo tofauti, wakiwemo watumishi kutoka taasisi za umma, mashirika binafsi, pamoja na wananchi wa kawaida wanaotaka kuboresha ujuzi wao wa kijamii katika maswala ya Kidipolomasia.

Washiriki wamepata fursa ya kipekee ya kufundishwa na mwanadiplomasia mbobezi, Balozi Peter Kalaghe ambapo katika darasa la leo, amesisitiza umuhimu wa itifaki na ustaarabu kama nguzo kuu ya mawasiliano yenye tija na uhusiano bora wa kikazi, iwe ndani au nje ya nchi.