Uongozi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR) umemkaribisha na kufanya mazungumzo rasmi na Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih, katika ziara yake ya kutembelea taasisi hiyo.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili fursa mbalimbali za ushirikiano wa kidiplomasia na kielimu kati ya Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.Salim Ahmed Salim na Visiwa vya Comoro.
Aidha, Mheshimiwa Balozi alieleza dhamira ya kuendeleza ushirikiano wenye manufaa kwa nchi zote mbili, huku akisisitiza nafasi muhimu ya elimu ya diplomasia katika kukuza mahusiano ya kimataifa na maendeleo ya kikanda.
Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za CFR za kuimarisha ushirikiano na wadau wa kimataifa katika kukuza diplomasia, elimu, na mahusiano ya kimataifa
DAR ES SALAAM: Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Sa...
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim ( CFR), kimetoa wito...
Mafunzo ya muda mfupi kuhusu Itifaki za Mashirika na Uhusiano wa Serikali (Corpo...
Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania, Mheshimiwa Yordenis Despaigne Vera, l...
Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, kimepokea ujumbe kut...